Searching...
Jumatano, 5 Februari 2014

WATOTO WACHANGA WAKEKETWA WILAYANI MANYONI



Watoto wachanga.
Wilaya ya Manyoni mkoani  Singida imetajwa kukeketa watoto wachanga, hali ambayo inasababisha vitendo hivyo kushindwa kutokomezwa, licha ya kuwa na madhara makubwa kwa afya.

Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji  wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),  Imelda Urio alisema hayo Dar es Salaam  jana wakati akitoa tamko  la  kupinga ukeketaji duniani, ambayo itaadhimishwa keshokutwa katika kijiji cha Ngimu, mkoani Singida. 
 
"Vilevile taarifa zinazoonesha kwamba katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwepo na ukeketaji unaofanywa kwa watoto wachanga hasa katika wilaya ya Manyoni mkoani Singida," alisema Imelda ambaye alikuwa akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa LHRC, Dk. Hellen Kijo-Bisimba.
 
Kuhusu takwimu za watoto wachanga wanaofanyiwa vitendo hivyo,  alisema ni vigumu kuzipata, kwani mashirika yanayopinga ukeketaji yalianza ukaguzi kwa watoto, ambapo  wanawake waliambiwa watoto wao wakaguliwe wanapokwenda kliniki kwa ajili ya chanjo mbalimbali, lakini wazazi waligoma kuwapeleka  watoto huko.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!