Searching...
Alhamisi, 6 Februari 2014

WALIOTEKA MAGARI WATUPWA JELA MIAKA 90


MAHAKAMA ya Hakim Mkazi wilaya ya Nzega mkoani Tabora imewahukumu watu watatu kwenda Jela miaka 90 kwa kubainika na kosa la Unyanganyi wa kutumia silaha kuwapora Milioni 18 ambapo ni kinyume na kifungu cha 287 cha sheria ya kanuni ya adhabu.

Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi Silvester Kainda, baada ya kusikiliza ushahidi wa mashitaka kwa washitakiwa watatu kati ya watano,ushahidi umethibitisha bila kuacha shaka kuwa Antony Joseph,Charles Richard na Samweli John wamehukumiwa kwenda jela miaka 90 huku kila mmoja akitumikia miaka 30 jela.

Awali ya hapo Mwendesha mashitaka wa Jeshi la Polisi mkaguzi msaidizi Mellito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo Aprili 2 mwaka 2013 watuhumiwa watano waliotuhumiwa kwa kuteka wafanya biashara walio kuwa wakienda mnadani Mambali na kupora milioni 18.

Ameiambia mahakama hiyo kuwa majambazi hayo yakitumia silaha aina ya Bunduki SMG 1 yalifanikiwa kupora fedha hizo za wafanya biashara.

Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi Mellito Ukongoji aliwataja waliokamatwa na tukio hilo kuwa ni Samweli John(35) mkazi wa Nzega nyasa,Joseph Kisumo,Mkwangu Masaniwa(30) mkazi wa Ngukuno pamoja na Charles Nkazi
(25) wa Kosangati Kibondo Kigoma na Charles Richard mkazi wa Kipilimuka.

Washitakiwa watatu kati ya watano wamekumbwa na hukumu hiyo ya miaka 90 jela ambao ni Antony Joseph, Charles Richard na Samweli John huku washitakiwa wawili wakiachwa huru baada ya kutobainika na hatia ya utekaji ambao ni Joseph Kisumo na Mkwangu Masaniwa.

Melito  ameiambia mahakama hiyo kuwa itoe adhabu kali ili iwefundisho kwao na kwa jamii hata hivyo washitakiwa hao watatu walipewa nafasi ya kujitetea hawakujitetea badala yake waliiomba mahakama hiyo iwapatie nakala ya hukumu zao.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!