Searching...
Jumatatu, 17 Februari 2014

TUZO ZA KILI 2014 ZAZINDULIWA LEO-YAFANYA MABORESHO MAKUBWA.

Screen Shot 2014-02-17 at 10.54.08 AM
GEORGE KAVISHE.
Huu ni muda wa kufahamu kuhusu tuzo ambazo hutolewa kwa Wanamuziki/Wasanii mbalimbali wa Tanzania zikiwa zimeanzishwa mwaka 1999 ambapo za mwaka huu 2014 zimezinduliwa leo February 17.
George Kavishe kutoka TBL ambao ndio Wadhamini wa tuzo hizi amesema >>> ‘Maboresho makubwa ambayo tumefanya mwaka huu ni tofauti na mara zote ambazo tumekua tukihusisha Watanzania dakika za kupiga kura tu hivyo wanakosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye category gani, mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani’
‘Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za kupigiwa kura na Wananchi, Watanzania watatuma kura zao kupitia simu ya mkononi kupitia 15440, unapendekeza msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye kipengele’ – Kavishe
‘Kwa hiyo Mwaka huu Watanzania watapiga kura mara mbili ambapo ya kwanza ni nani aingie kwenye category alafu tutarudi tena kupiga kura nani awe mshindi wa kwanza, yani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya Waandishi, Watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama wimbo uliopendekezwa na Wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia KTMA’ – Kavishe

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!