MARIO BALOTELI.
Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger amesema yupo tayari kutoa kitita kikubwa cha fedha ili kumsajili mshambuliaji mtukutu wa Italia anayekipiga na klabu ya AC
Milan Mario Balotelli, 23, baada ya kufanya mazungumzo ya mafanikio na wakala wa mchezaji huyo.
MARIO MANDZUKIK.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema yupo tayari kutoa kitita cha paundi milioni 25 ili kuinasa saini ya mshambuliaji nguli wa Bayern Munich,27 Mario Mandzukic.
WILLIAM CARVALHO.
Manchester United wamesema wamemfanyia uchunguzi mara kumi na mbili msimu huu kiungo kinda wa Sporting Lisbon William Carvalho ambapo wamesema wapo tayari kumsajili mwishoni mwa msimu huu baada ya kuridhishwa na kiwango chake.
0 comments:
Chapisha Maoni