Meneja Mauzo wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ilala, Jesca Njau (kushoto)
akikata utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi wodi ya watoto wachanga
Katika Hospitali ya Rufaa ya Amana Ilala iliyokarabatiwa kwa msaada
kampuni hiyo, Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Daktari
Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala, Mhandisi wa
TBL, John Malisa na Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Meshack Shimwela.
TBL ilitumia sh. mil. 68 kukarabati wodi hiyo na miundombinu yake.
Jesca Njau akipongezwa na Daktari Bingwa wa Watoto wa Hospitali hiyo, Dk. Mtagi Kibatala,
Dk. Kibatala
akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo ambao alidai umepunguza kwa
asilimia kubwa kupunguza adha kwa wazazi waliozaa watoto njiti.
Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo, Dk. Shimwela akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo
mkubwa wa ukarabati wa wodi ya wazazi na miundombinu ya maji.
Ofisa Uhusiano
wa TBL, Doris Malulu akielezea mikakati ya kampuni hiyo katika kusaidia
jamii katika sekta ya maji, ambapo katika mkoa wa Dar es Salaam TBL
imetumia sh. mil 450 kuboresha sekta ya maji katika vituo mbalimbali vya
afya.
Mzazi
alyejifungua mtoto njiti Mariam Mbwambo, akitoa shukurani kwa TBL kwa
msaada huo ambao alisema umesaidia kupunguza kero waliyokuwa wanaipata
kukaa na watoto hao ambao wanahitaji uangalizi mkubwa.
Mkazi wa Msimbazi Bondeni, Febi Joramu akitoa shukrani kwa TBL kwa msaada huo muhimu wa wazazi.
Jesca Njau akizungumza na Mariamu baada ya kukabidhi eneo hilo lililokarabatiwa.
Moja ya vyoo vilivyokarabatiwa
Sehemu ya mabomba yiliyokarabatiwa
Muuguzi Kiongozi wa Wodi ya Wazazi, Mercy Maleko akionesha choo kilichokarabatiwa cha watumishi wa wodi hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni