Polisi nchini Venezuela wamekabiliana na waandamanaji
wa upinzani katika barabara za mji mkuu wa Carcas ambao wanataka
kuachiliwa huru kwa wanafunzi waliokamatwa wiki iliopita.
Polisi wa kukabiliana na ghasia walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya huku waandamanaji hao wakiwatupia mawe.
Awali maelfu ya wafuasi wa Rais
Nicholas Maduro pia walishiriki katika maandamano ya kuwapinga
waandamanaji hao katikati mwa mji mkuu wa Carcas.
Rais Maduro ameushtumu upinzani kwa kuzua fujo kwa lengo la kutaka kuipindua serikali yake.
Watu watatu waliuawa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali siku ya jumatano.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John
Kerry ,ametoa taarifa akiitaka serikali ya bwana Maduro kuwaachilia
huru wafungwa wote waliokuwa wakiandamana mbali na kuheshimu uhuru wa kujieleza
0 comments:
Chapisha Maoni