Searching...
Jumamosi, 8 Februari 2014

LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU KURASA ZENYE JINA LAKE FACEBOOK,TWITTER NA INSTAGRAM



WAZIRI MKUU WA ZAMANI MH.EDWARD LOWASSA.
Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la Mhe. Edward Lowassa katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter, Instagram n.k. zinaonekana mmiliki wake ni Mhe. Edward Lowassa.

Ukweli ni kwamba hizo zote hazimilikiwi na Mhe. Lowassa.
Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo  hazihusiani kwa namna yoyote na Mhe Lowassa.
Hata hivyo Mh Lowassa anawashukuru wote wenye kumiliki account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.
Imetolewa na Ofisi ya Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (MB)

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!