Searching...
Jumanne, 25 Februari 2014

KIMENUKA CHADEMA,TAARIFA KAMILI YA MADIWANI KUJIUZULU HII HAPA

 MH.FREEMAN MBOWE MWENYEKITI WA CHADEMA TAIFA

Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Shinaynga kimepata pigo kubwa baada ya madiwani wake wawili katika manispaa ya Shinyanga kutangaza kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na madai kuwa  viongozi wa ngazi ya taifa  wa chama hicho kuendekeza  majungu,migogoro ,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwapa majina ya wasaliti wa chama.
Madiwani  waliofikia maamuzi hayo magumu ni diwani wa Kata ya Ngokolo Sebastian Peter maarufu OBAMA WA NGOKOLO na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo  ambao wamesema wameamua kufikia maamuzi hayo magumu kama ishara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa.
Madiwani hao wawili tayari wameshakabidhi barua za kung’atuka nafasi zao katika ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga
Hili   ndiyo barua ya tamko la diwani wa Ngokolo Sebastian Peter kuhusu kujiuzulu nafasi yake ya udiwani aliyoikabidhi ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga ikieleza sababu za kuchukua maamuzi hayo huku akisisitiza kuwa atabaki kuwa mwanachama mwadilifu wa Chadema

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!