Searching...
Jumatatu, 3 Februari 2014

ASKARI POLISI WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA GARI WAAGWA MKOANI DODOMA TAYARI KWA MAZISHI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akizungumza kwa Masikitiko wakati wa kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gariKamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma,Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME akiongoza waombolezaji kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gariMiili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ikiwa imebebwa
Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans wameagwa Mkoani Dodoma tayari kwa mazishi.
Akiongea kwa masikitiko Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME amewashukuru watu waliojitokeza kuungana pamoja kuaga miili ya Askari hao
Pia amewataka madereva wote kuwa waangalifu wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kujitokeza za namna hii.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!