Mchezaji wa Bayern Munich Thomas Muller akishangilia pamoja na wenzake goli lake aliloifungia timu yake likiwa ni goli la kwanza huku wachezaji wa Arsenal wakionekana wakiwa hoi baada ya kutandikwa mabao 2-0 na wajerumani hao na kuwaweka njia panda ya kuendelea na michuano hiyo mikubwa barani ulaya.
Mwamuzi Nicola Rizzola akimzawadia kadi nyekundu golikipa wa Arsenal Wojciech Szczesny baada ya kubainika kumchezea rafu mbaya mshambuliaji wa pembeni wa Bayern Munich Arjen Robben anayeonekana akigalagala chini.
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akimlalamikia na kumlaumu mchezaji wa Bayern Munich Arjen Robben kwa madai kwamba amejiangusha katika eneo la hatari na kumsababishia gilikipa wa Arsenal Wojciech Szczesny kulimwa kadi nyekundu.
Mchezaji tegemeo wa Arsenal Mesut Ozil akipoteza penalt baada ya kupiga penalt mbovu na mpira kupanguliwa kirahisi na mlinda mlango wa Bayern Munich,kitendo ambacho kimeifanya Arsenal kupoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani dhidi ya wajerumani Bayern Munich
Mchezaji wa Bayern Munich David Alaba akikosa penalti baada ya kupiga mpira na kugonga mlingoti wa goli na mpira kutoka nje.
Kiungo wa kimataifa wa England na Arsenal Jack Wilishere akiwa haamini macho yake baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa kuashiria kumalizika kwa pambano lao huku wakiwa wamebugizwa mabao 2-0 na miamba ya soka ya Ujerumani Bayern Munich katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates
Kufungwa kubaya,kocha wa Arsenal akitoka uwanjani kichwa chini baada ya kufungwa 2-0 na wababe wa soka wa Ujerumani Bayern Munich na kumuweka njia panda mzee huyo wa ufaransa pale atakaposafiri hadi ujerumani kurudiana na vijana hao wa Ujerumani.
Wakati mzee Arsene Wenger akitoka kichwa chini kijana wake kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alikua akikenua meno nje ikiwa ni muendelezo wa kuifunga timu hiyo ya London tangu kipindi akiwa anaifundisha Barcelona.
Mchezaji wa Bayern Munich Thomas Muler akiifungia timu yake goli safi la kichwa dakika ya 90 na kuifunga mdomo Arsenal 2-0
Ushindi rahaaaaaaa....tushangilie pamoja
kiungo mshambuliaji aliyetokea benji Thomas Muler akishangilia goli lake aliloifungia timu yake ya Bayern dakika ya 90 ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuingia uwanjani
Heka heka langoni mwa Arsenal.
0 comments:
Chapisha Maoni