Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akipokea Zawadi ya Ua wakati
akipokewa na Wafanyakazi wa Wizara hiyo jijini Dar leo,Tukio hilo
limefanyika Nje ya Wizara ya Fedha ambapo mamia ya Wafanyakazi asubuhi
ya leo walijitokeza Kuwalaki Mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Kikwete
wiki iliyopita ili kujaza nafasi za Mawaziri wanne zilizokuwa Wazi
kutokana na Kujiuzulu pamoja na Kifo cha Waziri wa Fedha Marehemu
Mgimwa.
Mh:Malima
ambaye ni Naibu waziri wa Fedha akipokea Zawadi ya Ua wakati wa
alipofika Rasmi Ofisini hii leo kwaajili ya Kuanza Majukumu yake baada
ya Kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Fedha.
Mapokezi yakiendelea asubuhi ya leo Nje ya Wizara ya Fedha.
Mapokezi
Yanaendelea,Watumishi wa Wizara ya Fedha walijitokeza Kwa wingi
kuwapokea Manaibu Waziri wapya wa Wizara hiyo.(Mh:Mwigulu Nchemba na
Mh:Adam Malima) Pembeni (Kushoto) ni Mkurugenzi wizarani hapo
aliyeongoza mapokezi hayo
Naibu Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akilakiwa na Maofisa wa
Wizara ya Fedha mapema hii leo asubuhi wakati alipofika Ofisini hapo
rasmi kuanza kazi.
Naibu
Waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba akibadilishana Mawazo na Katibu Mkuu
wa Wizara ya Fedha wakati wa hafla ya Kuwapokea Mawaziri hao Wapya hii
leo zoezi lililofanyika Wizara ya Fedha na Kukamilika Jioni ya Leo.
0 comments:
Chapisha Maoni