WAYNE ROONEY.
Kocha wa Manchester United David Moyes amesisitiza kwamba kamwe hawezi kuruhusu klabu imuuze mshambuliaji wake nguli Wayne Rooney, 28, kwenda Chelsea kama kocha wa Chelsea the Blues mreno Jose Mourinho anavyojipanga kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa England.
FABIO COENTRAO.
Uwezekano wa Manchester United kumsajili beki wa Real Madrid Fabio Coentrao, 25, ni mkubwa baada ya taarifa za ndani kutoka Madrid kueleza kwamba matajiri hao wa Hispania wanataka kumsajili beki wa Sevilla Alberto Moreno, 21.
DIEGO DE GIROLAMO.
Timu nne za ligi kuu soka England za Manchester City,Manchester United,livepool na Everton wapo vitani kuwania saini ya mchezaji wa Sheffield United mshambuliaji Diego De Girolamo, 18.
CHRISTIAN TELLO.
vijogoo vya Anfield Liverpool vitalazimika kusubiri hadi mwishoni mwa msimu huu kumsainisha mshambuliaji wa Barcelona Christian Tello,22 baada ya mshambuliaji huyo wa Hispania kuweka wazi kwamba anataka kusalia Nou Campo mpaka mwishoni mwa msimu huu.
LACINA TRAORE.
Everton wanaweza wakawazidi kete West Ham kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Monaco Lacina
Traore. Wagonga nyundo hao wa London walishamtafutia mchezaji huyo kibali cha kufanya kazi England lakini hawajaonyesha msisitizo wa kumsainisha.
MUNIR EL HADDADI.
Arsenal wapo kwenye mawindo makali ya kumsajili mshambuliaji kinda wa Barcelona Munir El Haddadi, 18, japokuwa itawalazimu kuongeza juhudi kwani kinda huyo anayedaiwa kuwa na kipaji cha hali ya juu pia anawindwa na Paris St-Germain na Bayern Munich
TETESI ZINGINE (SIO ZA UHAMISHO)
JOSE MOURINHO.
kocha wa Manchester United David Moyes amesema amepokea taarifa ya msamaha kutoka kwa kocha wa Chelsea Jose Mourinho kutokana na taarifa alizozitoa mreno huyo kwamba anazo taarifa za ndani za Man U kwamba watu wengi ndani ya timu hiyo hawana raha kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo mzunguko wa kwanza wa ligi kuu England.
ARSENE WENGER.
Imeelezwa kwamba Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anatarajiwa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuinoa timu hiyo ambapo mkataba wake wa sasa unatarajiwa kuisha mwishoni msimu huu.
EDEN HAZARD.
Kiungo mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard amesema anaamini siku moja atakuja kuwa mchezaji bora wa dunia,kauli ambayo imeungwa mkono na wengi na kumshauri aongeze tu bidii na kuwa na nidhamu ya soka ndani na nje ya uwanja.
0 comments:
Chapisha Maoni