ERIK LAMELA.
Mchezaji wa Tottenham Erik Lamela
anaonekana kufikia ukingoni kukipiga na miamba hiyo ya soka baada ya baba yake
kuweka wazi kwamba mwanae anataka kuondoka White Hart Lane. Mshambuliaji huyo
alijiunga na Spurs msimu uliopita kwa kitita kikubwa cha paundi milioni 30 na
kuweka rekodi klabuni hapo.
ALVARO MORATA.
Arsenal wanaonekana kuongeza
juhudi za kuipata saini ya mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 21, kwa
mkopo wa muda mrefu.
SUPER MARIO BALOTELLI.
Mshambuliaji mtukutu wa AC Milan super
Mario Balotelli, 23, ametupilia mbali na kupuuzia taarifa zinazoenezwa na vyombo
mbalimbali vya habari Italia kwamba ana mpango wa kuihama timu yake mwezi huu.
NEMANJA VIDIC.
Beki kisiki wa Manchester United Nemanja Vidic amesema
anataka kuondoka Old Trafford mwishoni mwa mwa msimu huu,kwa sasa Vidic
amesalia na mkata wa miezi sita tu kunako Manchester United na wakala wake
amesema tayari anazo ofa nzuri za timu za Italia Serie A lakini hakuitaja ni
timu gani japo watu wanadai anataka kutimkia Inter au Ac Millan.
ANDREA PIRLO
Kiungo mkongwe Andrea Pirlo 34 yupo
tayari kuingia mkataba mpya wa miaka miwili na timu yake ya kibibi kizee cha
Turin Juventus.
JAY BOTHROYD
Mchezaji wa zamani wa timu ya
taifa ya England na Queens Park Rangers mshambuliaji Jay Bothroyd amesaini
kandarasi ya paundi milioni 5 kukipiga na
tumu ya Muangthong United ya nchini Thailand.
MOHAMED SALAH.
Timu ya Zenit St Petersburg ua
Urusi ipo mbioni kuwazidi kete Liverpool, Manchester United na Tottenham kuinasa
saini ya mshambuliaji wa timu ya Basle Mohamed Salah 21.
CRAIG GARDNER.
West Bromwich Albion wanataka kumsajili kiungo wa
Sunderland Craig Gardner,kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 27 anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu ambapo kama
hawatamuuza sahivi basi ataondoka bure mwishoni mwa msimu.
0 comments:
Chapisha Maoni