SOLOMON KALOU
Timu za Liverpool na Spurs kwa pamoja zipo katika vita ya kuipata saini ya kiungo mshambuliaji wa zamani wa chelsea ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ivory Cost Salomon Kalou, 28, ambaye kwa sasa anakipiga na timu ya Lille ya Ufaransa.
MARIO MANDZUKIC.
Mshambuliaji wa Bayern Munich Mario Mandzukic, 27 anawindwa vikali na Manchester United na Arsenal baada ya timu yake kuweka wazi kwamba
mfumania nyavu Robert Lewandowski atajiunga na miamba hiyo ya Ujerumani kutokea kwa mahasimu wao Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu huu,kitendo ambacho kitamuweka benji Mandzukic.
RAHEEM STERLING
Kocha mkuu wa liverpool Brendan Rodgers amekanusha vikali taarifa kwamba ana mpango wa kumuuza mshambuliaji wake kinda Raheem Sterling 19.
0 comments:
Chapisha Maoni