Searching...
Jumatatu, 6 Januari 2014

HII NI AIBU KUBWA KWA MANISPAA YA KINONDONI KWENDA LIKIZO NA KUSAHAU MAJUKUMU

Huu ni mti mkubwa ulioanguka katikati ya barabara ya TRA mwenge jijini DSM na kusababisha foleni kubwa kutwa nzima ya jumapili 05/01/2014 huku viongozi mbali mbali wa manispaa ya kinondoni wakipita katika eneo hilo na kupuuzia adha wanayoipata wananchi.
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa,foleni kubwa iliyosababishwa na mti huo mkubwa ulioanguka kati kati ya barabara ya TRA mwenge jijini DSM kutokana na kusubiriana kupita kwenye kiuchochoro kidogo kutokana na mti huo kuziba njia.
 ilikua ni balaa kwa madereva.
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jumapili mchana katika barabara ya TRA Mwenge.
 Jambo la kushangaza kama sio kusikitisha,timu ya MCHOME BLOG iliporejea ktika barabara hiyo usiku wa saa saba uliukuta mti huo ukiwa bado haujaondolewa,na baadhi ya wafanyibiashara waliozungumza na mchome blog walisema wahusika (manispaa ya kinondoni) bado wapo likizo ya mwaka mpya.
 foleni ya kizembe usiku wa manane,kisa watu hawataki kuwajibika katika majukumu yao.
AIBU YENU WAHUSIKA,INGEKUWA BUNGENI NINGEOMBA MWONGOZO WA SPIKA KWAMBA KWANINI WAHUSIKA WASIJIPIME WAKAWAJIBIKA KAMA WALIVYOWAJIBIKA WALE WAHESHIMIWA MAWAZIRI WANNE.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!