Searching...
Jumapili, 5 Januari 2014

TETESI ZA UHAMISHO BARANI ULAYA,CHELSEA WAENDELEA KUICHOKONOA MAN U.

 
WAYNE ROONEY.
Katika hali ya kuonyesha kama ni kutangaza vita Chelsea wameendelea kuichokonoa Manchester United baada ya kuweka wazi kwamba wapo tayari kutuma ofa ya paundi milioni 30 ili kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa England Wayne Rooney, 28, endapo mchezaji huyo atakataa kuingia mkataba mpya na mashetani hao wekundu.
Papy Djilobodji 
 PAPY DJILOBODJI.
Wakati huo huo Chelsea wapo katika mawindo makali kwaajili ya kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Senegal ambaye pia anakipiga katika klabu ya Nantes kiungo wa kati  Papy Djilobodji, 25.
Bluebird bound? Zaha could be on the move to south Wales 
WILFRED ZAHA.
Mshambuliaji kinda wa Manchester United Wilfred Zaha huenda akatimkia kunako timu ya Cadiff city baada ya kocha wa Caddif ambaye pia ni mchezaji nguli wa zamani wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer kuhitaji huduma ya kinda huyo kwa mkopo wa muda mrefu.
Reunion? Rafael Benitez got on well with Mata who performed superbly under him
 RAFAEL BENITEZ.
Kocha wa timu ya Napoli ya Italia Rafa Benitez ameweka wazi kwamba hawajatuma ofa yoyote kwa Chelsea kwaajili ya kiungo wao wa kimataifa wa Hispania Juan Matta kwasababu wanaamini hawawezi kumpata katika kipindi hiki cha dirisha dogo.
 No shortage of suitors: Mata is in demand but may be better off staying at Chelsea
 JUAN MATTA.
Benitez ambaye amewahi kumfundisha Matta kipindi alipoifundisha Chelsea kwa mpito amesema angependa kufanya kazi na kiungo huyo kwa mkopo lakini Chelsea hawawezi kukubali ombi hilo.
 Martinez: I'd love to sign for Arsenal
 JACKSON MARTINEZ.
Katika hali inayoonyesha ni pigo kubwa kwa Chelsea na neema kwa Arsenal,mshambuliaji tegemeo wa Porto ambaye Mourinho alijaribu kumsajili msimu uliopita kwa udi na uvumba mcolombia Jackson Martinez, 27, amepasua jipu na kuweka wazi kwamba anaipenda sana Arsenal na anatamani kujiunga nayo mapema mwezi huu.
 Available: Fabio Coentrao is up for grabs this January - could United make another move?
FABIO COENTRAO.
Malengo ya Manchester United kwa mchezaji wa Real Madrid yanaweza yakatimia baada ya klabu hiyo tajiri ya Hispania kuweka wazi kwamba mchezaji wao Fabio Coentrao anaweza akaondoka kwa kitita cha paundi milioni 12,kauli ambayo inaweza ikachangamkiwa mara moja na Manchester United kutokana na juhudi zao za kumnasa nguli huyo msimu uliopita kugonga mwamba,japo kama Man U watazembea wanaweza wakaambulia patupu baada ya Chelsea nao kummendea kinda huyo.
Fab target: Spurs are monitoring Juve striker Fabio Quagliarella
 FABIO QUAGLIARELLA.
 Daniel van Buyten of Munich battles for the ball with Mirko Vucinic
 MIRKO VUCININIC
Tottenham wapo katika mazungumzo na klabu ya Juventus kwaajili ya kuwasajili washambuliaji wake wawili kwa mpigo wakongwe Mirko Vucinic na Fabio Quagliarella, kwaajili ya kuziba pengo la Jermain Defoe.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!