MAREHEMU BWANAMDOGO |
MAZISHI
ya Mbunge wa Chalinze mkoa wa Pwani, Saidi Mwanamdogo yaliyokuwa
yamepangwa kufanyika kesho, katika Kijiji Cha Miono, Bagamoyo, sasa
yatafanyika kesho kutwa ili kutoa nafasi kwa Rais Jakaya Kikwete kuhudhuria
mazishi hayo.
Mazishi hayo yatafanyika siku hiyo kutokana na kusubiriwa
kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye
yupo nchini Uholanzi katika ziara ya kikazi.
Akizungumzia leo nyumbani kwa marehemu, Makondeko
Dar es Salaam, ambako ndipo msiba ulipo kwa sasa kabla ya kusafirishwa ijumaa,
asubuhi, Baba mdogo wa marehemu Omar Khalfan Nguya amesema baada ya Rais
Kupata taarifa hizo nje ya nchi ameomba
siku ya kuzika iahirishwe na kufanyika ijumaa wiki hii.
Amesema Marehemu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa tumbo
kwa muda mrefu hali iliyosababisha kuanzishiwa matibabu nchini india ambapo kwa
kudra za mwenyezi mungu mbali ya jitihada zilizofanywa na madaktari amefariki
dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Marehemu Said BwanaMdogo ameacha mjane na watoto sita huku
wawili kati ya hao wakiwa ni wa nje ya ndoa.
Wakati huohuo, Katibu wa CCM Mkoani Pwani Sauda Mpambalioto
amesema wamepokea msiba huo kwa mshtuko mkubwa na kukiri kubadilishwa kwa siku
ya mazishi.
Mpambalioto amesema mbali ya msiba huo pia jana, wamemzika mjumbe wa halmashauri kuu CCM Taifa MNEC kupitia Mkuranga, Rukia
Ally Msumi ambaye alipata ajali ya pikipiki ambayo ilisababisha kifo chake.
Naye mbunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema
msiba huo ni pigo kwake kwani walikuwa karibu na marehemu kwa kushirikiana
kikazi na kupeana mawazo ya kiutendaji.
Koka amesema Bwanamdogo alikuwa ni mtu mcheshi, msikivu
,asiye na majivuno ,alipenda kuzungumza na kila rika pasipo kuwa na majivuno
hali inayomfanya awe na kitu cha kuiga kwake.
Amesema kutokana na sifa alizokuwana nazo marehemu haina
budi akawa mfano wa kuigwa na wabunge wengine na kuwataka wabunge wote kwa
pamoja kushikamana na kuwa kitu kimoja ili kujenga nyumba moja bila ya
kubaguana .
0 comments:
Chapisha Maoni