Searching...
Ijumaa, 3 Januari 2014

MWILI WA MAREHEMU DR.MGIMWA KUWASILI KESHO JUMAMOSI,KISHA KUZIKWA JUMATATU,RATIBA KAMILI HII HAPA


 
 MAREHEMU DR.WILLIAM MGIMWA.
Mwili wa aliekua Waziri wa fedha na Uchumi Dr. William Mgimwa unatarajiwa kuwasili Dar es salaam Tanzania kesho Jumamosi Jan 4 2014 ukitokea Afrika Kusini kwenye hospitali aliyokua kalazwa.
  MH.WILLIAM LUKUVI
Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mazishi ambae ni Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu sera uratibu na bunge William Lukuvi amesema baada ya kuwasili Jumamosi hiyohiyo saa tano asubuhi ataagwa kwenye viwanja vya Karimjee Dar es salaam kabla ya kusafirishwa kuelekea Magunga Iringa kwa maziko January 6.
RATIBA KAMILI.
TAREHE 4/ 01/ 2013
 MWILI WA MAREHEMU UNATARAJIA KUWASILI UWANJA WA NDEGE WA JULIUS NYERERE TERMINAL II, SAA7: 00 MCHANA. BAADA YA KUWASILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWA MAREHEMU MIKOCHENI B.
2:- SAA 11:00 JIONI MWILI UTAPELEKWA HOSPITALI YA LUGALO.
TAREHE 5/ 01/ 2013
SAA 3:00 HADI SAA 4:00 ASUBUHI:- CHAKULA NYUMBANI KWA MAREHEMU.
SAA 4:30 ASUBUHI :- MWILI KUWASILI NYUMBANI MIKOCHENI B.
SAA 5:30 HADI SAA 8:00 MWILI UTAPELEKWA UKUMBI WA KARIMJEE KWA AJILI YA SHUGHULI ZA IBADA NA HESHIMA ZA MWISHO.
SAA 8:10 MWILI UTAPELEKWA UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU NYERERE TERMINAL I.
SAA 10:00 MWILI UNATARAJIA KUWASILI IRINGA UWANJA WA NDULI  NA KUAGWA KATIKA UKUMBI WA SIASA NI KILIMO-IRINGA
SAA 11:30 JIONI MWILI UTASAFIRISHWA KUELEKEA KIJIJI  CHA MAGUNGA.
TAREHE 6/ 01/ 2013 
SAA 6:00 MCHANA SHUGHULI ZA MAZISHI KIJIJINI KWA MAREHEMU MAGUNGA.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!