Searching...
Alhamisi, 23 Januari 2014

MRITHI WA JUAN MATA CHELSEA KUTUA RASMI LEO,NI KUTOKA FC BASEL,LIVEPOOL WAZIDIWA KETE NA MOURINHO

Blues confirm signing of 'new Messi'
MOHAMED SALAH.
Hatimaye masaa kadhaa baada ya klabu ya Chelsea kumuuza kiungo wao mshambuliaji Juan Mata kwa mashetani wekundu wa England Manchester United sasa wametangaza rasmi kwamba wamekubaliana na klabu ya FC Basel kwaajili ya kumsajili mshambuliaji wao wa pembeni Mohamed Salah ili kuziba pengo la muhispania Juan Mata.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri alikua ni chaguo la kwanza kwa klabu ya Liverpool na alikua katika hatua za mwisho kusaini kunako Anfield lakini Chelsea wamewazidi kete kama vile walivyofanya katika usajili uliopita baada ya kuwazidi kete Tottenham pale walipomsajili kiungo mshambuliaji Willian
Jose Mourinho has been after the player (Picture: AP)
JOSE MOURINHO.
‘Kinachosubiriwa sasa ni kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri kumalizana na Chelsea mafao yake pamoja na Vipimo kabla ya kutangazwa rasmi kuitumikia klabu hiyo ya tajiri wa Urusi Roman Abrahamovich’

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!