Searching...
Jumatano, 29 Januari 2014

MHE. JUMA NGASONGWA APATA AJALI KIBAHA PICHA YA NDEGE 28.01.2014

 Mh Juma Ngasongwa akikokotwa kuingizwa Hospitali ya Tumbi kupatiwa matibabu baada ya kupata ajali katika eneo la Kibaha jana jioni. Mhe. Ngasoma amenusurika kifo katika ajali hiyo iliyotokea jana jioni Kibaha Picha ya ndege Mkoani Pwani.
  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza na Dr Loti Kiwelu akimjulia hali katika Hospitali ya Tumbi Kibaha alipofikishwa kwa ajili ya huduma ya kwanza ambapo alihamishiwa katika Hosipitali ya Muhimbili MOI kwa ajili ya matibabu zaidi.

 Ajali hiyo ilihusisha gari  aina ya Rav 4 mali ya Ngasongwa ambaye alikuwa akiendesha mwenyewe kutoka jijini Dar es salaam kuelekea Morogoro ambapo kwa mujibu wa Ngasongwa alichomekewa na lori la Tanesco pichani chini.
 Lori la Tanesco lililosababisha ajali hiyo.
 Gari la Ngasongwa likiwa limeharibika vibaya. Picha na Chris Mfinanga.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!