Maisha ya Askofu wa Huduma ya Ngurumo ya Upako, Geor Davie anayevuma zaidi jijini Arusha na Dar es Salaam ni ya kifahari, anaabudiwa zaidi ya manabii na analindwa kuliko marais mbalimbali duniani.
Davie ambaye hujulikana zaidi kwa jina la Mtume, ana msafara mrefu kwenye ziara zake anazokwenda kutoa huduma ambao husheheni magari mengi ya kifahari kuliko marais wengi.
OneloveTz tuna mlolongo wa matukio ya Davie ambayo yanajieleza kwa picha ambazo zinabainisha namna mtumishi huyo wa Mungu anavyokula bata.
MSAFARA WA SHS. MIL. 200
Matukio yanaonesha kuwa, baadhi ya misafara ya Davie imekuwa na msururu mrefu wa magari ambayo hayapungui kumi.
Uchunguzi umeonesha kuwa, magari hayo, kila moja linanunuliwa kati ya shilingi milioni 20 na 40, hivyo thamani ya ‘mikoko’ peke yake inaleta wastani wa jumla ya zaidi ya shilingi milioni 200 bila ya mafuta ambayo nayo hugharimu fedha nyingi.
ULINZI DAH!
Kila sehemu ambayo Davie hufika kwa lengo la kutoa huduma, huzungukwa na walinzi kati ya nane na 10 ambao huvaa nadhifu, suti nyeusi na miwani nyeusi.
Walinzi hao, humzunguka Davie na kufanya anapotembea asikaribiwe na watu kwa urahisi, huku wakimuongoza hatua kwa hatua.
Habari zinadai kuwa walinzi hao wameajiriwa na Kanisa la Huduma ya Ngurumo ya Upako na hulipwa mishahara kwa ajili ya kumlinda kiongozi huyo.
GARI LAKE LINA BENDERA MBILI
gari la Davie ambalo hupambwa na bendera mbili kama ilivyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa kawaida, gari la rais hupambwa na bendera mbili, moja ikiwa ya taifa na nyingine ya rais.
Hata hivyo, blog hii halijapata ufafanuzi kuhusu bendera mbili za gari la Davie, ingawa waumini wake wanasema kwamba ni alama ya huduma ya kanisa lake.
NI RED CARPET KILA ANAPOKWENDA
Davie anaheshimiwa kwa kiasi kikubwa na waumini wa huduma ya kanisa lake, hivyo hutandikiwa zulia jekundu ‘red carpet’ kila anapokwenda kutoa neno, huku akizungukwa na walinzi wake.
FULL KUABUDIWA
Neno la Davie siyo tu kwamba linampa wafuasi bali pia kwa wengine humuabudu kwa imani kuwa amejaliwa ufunuo mkubwa wa matatizo ya binadamu aliopewa na Mwenyezi Mungu.
blog hili lina picha za watu wakisujudu na kumshika viatu kwa imani kwamba tendo hilo huwapa utakaso wa kiroho na matatizo mbalimbali.
SOURCE NA DJ SEK
0 comments:
Chapisha Maoni