Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima zao za
mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha,
marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo
zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam 05/01/2014
Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dk. William Mgimwa,
wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika
kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mjane wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, Mama Maria Nayerere akitoa heshima za mwisho
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt.
William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho
zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Spika wa Bunge Anna Makinda akitoa heshima za mwisho
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Dk. Mgimwa mjini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Dk. Mgimwa.
Wananchi mbalimbali waliofika kutoa heshima za mwishi kwa mwili wa Dk Mgimwa.
Viongozi kutoka baadhi ya vyama vya siasa, Mwenyekiti wa NCCR
Mageuzi, James Mabatia na Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba wakiwa
kwenye shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Dk. Mgimwa.
Waombolezaji kwenye kuaga mwili wa Dk, Mgimwa
Waombolezaji wakiwa Karimjee kuaga mwili wa Dk Mgimwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Jane Kakingo Mgimwa, mjane wa
aliyekuwa Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa baada ya mwili wa marehemu
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Nduli Iringa Desemba 5, 2014 kwa
ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kijijini Magunga Desemba 6,
2014.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akishuhudia wakati mwili wa aliyekuwa
Waziri wa Fedha, Dr. William Mgimwa wakati ulipowasili kwenye uwanja wa
ndege wa Nduli Iringa Desemba 5,2014 kwa ajili ya mazishi
yanayotarajiwa kufanyika Desemba 6, 2014 kijijini Magunga.
0 comments:
Chapisha Maoni