Searching...
Jumanne, 7 Januari 2014

HII NDIYO SARAFU YA KUMBU KUMBU YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI,YAKABIDHIWA RASMI KWA MAKAMU WA RAIS

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (kushoto) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu baada ya kukabidhiwa Sarafu maalum ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito wa g 16, baada ya kukabidhiwa Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (katikati) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014 kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka (katikati) na Mshauri wa masuala ya Sarafu, Hassan Jarufu, wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014 kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu ya Kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiitazama  Sarafu ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Mapinduzi yenye uzito ya g 16, baada ya kuipokea kutoka kwa Meneja wa Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Jovent Rushaka wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jan 7, 2014 kwa ajili ya kumkabidhi Sarafu hiyo. 

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!