Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi cheti kwa Meneja
Rasilimali Watu Uhusiano wa Kibiashara (HR Business Partner) wa Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Emmanuel Christopher (kulia), baada ya
kampuni hiyo kupata tuzo ya utoaji mafunzo na maendeleo kwa wafanyakazi
yakiwemo ya elimu ya jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Ukimwi. Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Bw. Almas
Maige, Waziri wa Kazi na Ajira, Bi Gaudentia Kabaka na Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa (ILO), Bw. Guy Ryder. Hafla hiyo
ya kukabidhi tuzo kwa waajiri bora ilifanyika Dar es Salaam mwishoni mwa
wiki.
Jumapili, 8 Desemba 2013
Related Posts
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
0 comments:
Chapisha Maoni