Searching...
Jumamosi, 7 Desemba 2013

MAKUNDI YA MICHUANO YA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA BRAZILI YAPANGWA,NCHI ZA AFRIKA HALI NGUMU

England face nightmare World Cup group
Hapana shaka wapenzi wa soka barani Afrika pamoja na kuomboleza kifo cha Nelson Mandela wamekuwa wanafuatilia Droo ya kombe la dunia kufahamu nani wapinzani wa timu tano zinazowakilisha bara hilo.

Cameroon wamejikuta katika kundi gumu la A pamoja na wenyeji Brazil, Mexico na Croatia.

Mabingwa watetezi Uhispania watakuwa katika kundi B pamoja na Netherlands waliokutana nayo fainali kombe lililopita, na timu zingine ni Chile na Australia.

Dua ya Ivory Coast ya kuepuka kundi gumu sana wakati huu inaonekana imesikika, wako katika kundi C pamoja na Colomboa, Japan na Ugiriki.
England face nightmare World Cup group 
KOCHA WA ENGLAND ROY HODGSON.
England watakuwa na kibarua kigumu kwenye kundi D ambapo wapinzani wao ni Italia, Uruguay na Costa Rica.

Kwenye kundi E Ufaransa inacheka usiku huu kwani imepangwa pamoja na Uswizi, Ecuador na Honduras.Mabingwa wa Afrika Nigeria wako katika kundi F pamoja na Argentina Iran na Bosnia Harcegovinia, ambayo inashiriki kombe la dunia mara ya kwanza.

Ghana ndiyo inayoonekana kuwa matatizoni miongoni mwa timu za Afrika. Wamejikuta katika kundi G ambapo watapamaba na na Ujerumani, Marekani na Ureno.Timu ya tano ya Afrika Algeria itakuwa kwenye kundi H na wapinzani hapo ni Ubelgji, Korea Kusini na Urusi.
MAKUNDI KAMILI HAYA HAPA.
Group A: Brazil, Cameroon, Mexico, Croatia
Group B: Spain, Chile, Australia, Holland
Group C: Colombia, Ivory Coast, Japan, Greece
Group D: Uruguay, Italy, Costa Rica, England
Group E: Switzerland, Ecuador, Honduras,France
Group F: Argentina, Nigeria, Iran, Bosnia
Group G: Germany, Ghana, USA, Portugal
Group H: Belgium, Algeria, South Korea, Russia

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!