Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Nelson Mandela Mandela.
Mji wa Johannesburg umemiminika watu
waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii,
familia na marafiki wao.
Viongozi duniani pia wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.....
Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi
saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa
Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama
mtoto wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.
Je uko Afrika Kusini? Unaweza kututumia picha au
video kuhusu yanayojiri huko na tutayaweka hapa kwenye mtandao wetu.
Tutumie picha au ujumbe wako wowote kupitia ukurasa wetu
waFacebookbbcswahili
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Na wewe pia unaweza kutuma ujumbe wako kupitia
ukurasa wetu wa Bofya Facebook ambao kisha nitauweka kwenye mtandao wa
Bofya bbcswahili
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa Mzee
Mandela, miongoni mwa wengine kama Oliver Tambo, Govan Mbeki na
wengine, walijitlea maisha yao na ujana wao wote katika kupigania haki
na kuikomboa Afrika Kusini. Walijivunia kweli walichoamini na
wakatekeleza. Sasa ni jukumu letu na wadogo wetu kuendeleza kazi ya
Mandela.''
Rais wa Malawi Joyce Banda, "Wakati kama huu,
sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea, lakini ni huzuni
kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa kumpoteza
kijana wa Afrika Dr.
Nelson Mandela kwasababu vita alivyopigana sio
tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji wa aina
yoyote dhidi ya binadamu.
Na ndio maana vijana, na wazee, wake kwa waume,
weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu
alivyopigania."
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa
Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi
Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani.
Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine
wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka
yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.
Katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko,
amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana
mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."
NA BBC SWAHILI
0 comments:
Chapisha Maoni