Searching...
Jumanne, 10 Desemba 2013

HIVI NDIVYIO MISA YA WAFU YA KUMUOMBEA MZEE NELSON MANDELA INAVYOENDELEA HIVI SASA KATIKA UWANJA WA SOCCER CITY JIJINI JOHENNESBURG

 Rais wa Marekani, Barack Obama na Mke wake wakisoma kitabu cha ratiba ya misa ya kumuombea rais wa zamani wa Afrika ya Kusini  Nelson Mandela aliyefariki akiwa na umri wa miaka 95.
 Mke wa Marehemu, Graca Machel akiwa kwenye hali ya uzuni wakati wa misa ya kumuombea marehemu Nelson Mandela aliyekuwa rais wa zamani wa Afrika ya kusini.
 Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela . Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB. Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili. Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
 Rais wa Afrika ya Kusini, Jacob Zuma alipowasili kwenye uwanja First National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani. Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu. Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini
ENDELEA KUTIZAMA MATUKIO ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA CHINI
 Rais wa Brazil Dilma Rousseff (kulia) akiwasili kwenye uwanja wa First National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela: Watu wengi wamekaidi hali mbaya ya hewa ambapo mvua kubwa imenyesha huku wakikusanyika uwanjani humo wakisubiri kwa muda mrefu kabla ya misa hiyo kuanza muda mfupi uliopita. Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Mjukuu wa rais wa zamani,  Mandla Mandela akiwa kwenye uwanja wa First National Bank (FNB) kwa ajili ya maombezi ya mwili wa rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!