Searching...
Jumanne, 10 Desemba 2013

WAHABESHI 56 WAKAMATWA WILAYANI SAME, MKOANI KILIMANJARO KWA KOSA LA KUINGIA NCHINI BILA KIBALI

Sehemu ya wahamiaji haramu 56, Raia wa Ethiopia waliokamatwa usiku wa kuamkia Jana, katika Kijiji cha Jiungeni, kata ya Ruvu, wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro, ambao wanaonesha kuwa na Njaa kutokana na kusafiri umbali Mrefu, wakiwa wanakula Maembe katika sehemu ya wazi Makao Makuu ya jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Ofisini Kwake, Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alisema Wahabeshi hao walikamatwa majira ya saa sita usiku, usiku wa kuamkia Juzi, wakiwa katika Lori aina ya Fuso, yenye namba za usajili, T188 AYU, mali ya kampuni ya E.Lyimo ya Mjini Moshi.
Lori aina ya Fuso, yenye namba za usajili, T118 AYU mali ya kampuni ya  E.Lyimo ya mjini lililokamatwa na Wahamiaji haramu 56, Raia wa Ethiopia katika kijiji cha Jiungeni, kata ya Ruvu, wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro likiwa limeegeshwa Makao Makuu ya jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.
Sehemu ya wahamiaji haramu 56, Raia wa Ethiopia waliokamatwa usiku wa kuamkia Jana, katika Kijiji cha Jiungeni, kata ya Ruvu, wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro, ambao wanaonesha kuwa na Njaa kutokana na kusafiri umbali Mrefu, wakiwa wanakula Maembe katika sehemu ya wazi Makao Makuu ya jeshi la Polisi Mkoani Kilimanjaro.
Kamanda Boaz alisema baada ya kupata taarifa ya uwepo wa watu wanaotiliwa mashaka kijijini hapo, polisi walianza kufuatilia na kuwahi Gari hilo likiwa na Wahamiaji hao ambao hata hivyo bado haijafahamika walikuwa wakielekea wapi.
“Polisi waliwahi baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi na kukamata wahabeshi 56, walikuwa wanasafirishwa kwenye Lori aina ya Fuso, namba za usajili T188 AYU mali ya E.Lyimo ya mjini Moshi, bado hatujafahamu walikuwa wanaelekea wapi lakini uchunguzi unaendelea,” alisema Boaz.
Kamanda Boaz alisema mbali na Wahabeshi hao 56, Polisi walifanikiwa kuwakamata Watanzania Watatu akiwemo Dereva wa Lori hilo, aliyetambulika kwa jina la Daniel Mfinanga pamoja na wenzake wawili ambao majina yao yanahifadhiwa kutokana na sababu za kiupelelezi.
Aidha Kamanda Boaz alioneza kuwa Utingo wa Lori hilo, aliyemtaja kwa jina la Ismael Juma, alifanikiwa kutoroka na kwamba jeshi hilo kwa sasa linaendelea na msako ili kumtia mbaroni.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!