Hatimaye mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Porto ya Ureno ambaye amekua akitolewa macho na klabu ya chelsea Jackson Martinez ameweka wazi nia yake ya kuondoka ureno na kutaka kuhamia England katika kipibdi cha usajili wa dirisha dogo januari mwakani ambapo amesema anataraji kupata uhamisho mzuri.
Martinez ndilo lilikua chaguo la pili nyuma ya Wayne Rooney kipindi cha usajili lakini Mourinho akajikuta akidondokea pua na kuishia kumsajili mkameroon Samuel Etoo kwa mkataba mfupi wa mwaka mmoja.
Uhamisho wa Martinez kwenda Chelsea utakua ndio mwisho wa enzi za Demba Ba ambaye ameonekana kutokuwa chaguo la Mourinho.
pamoja na hayo lakini haitakuwa kazi rahisi kwa chelsea kumpata Martinez kutokana na matajiri wengine wa Borussia Dortmund, Monaco na Napoli kumtaka pia mfumania nyavu huyo.
0 comments:
Chapisha Maoni