Searching...
Jumatano, 13 Novemba 2013

JE WAJUA KOCHA WA ZAMANI WA CHELSEA ROBERTO DE MATEO ANAENDELEA KULIPWA MSHAHARA HADI MWAKANI??

Roberto Di MatteoRoberto Di Matteo
 ROBERTO DE MATEO AKISHANGILIA KOMBE LA KLABU BINGWA ULAYA ENZI ZA UKOCHA WAKE CHELSEA
Kocha wa zamani wa Chelsea Roberto Di Matteo pamoja na kwamba alifukuzwa kazi ndani ya klabu hiyo lakini bado anaendelea kulipwa mshahara wake mnono ambapo kila wiki analipwa paundi 130,000.
Muitaliano huyo alishindwana na tajiri wa kirusi ambaye ndiye mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich na kukatisha mkataba wake wa miaka mitatu baada ya miezi sita tu baada ya kuipatia klabu hiyo taji la klabu bingwa ulaya kwa mara ya kwanza na kuweka historia
Kutokana na malipo hayo Di Matteo anajiingizia kiasi cha paundi milioni 7 kila mwaka hadi mkataba wake utakapoisha mwezi wa sita mwaka 2014.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!