Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa Chama
cha ANC cha Afrika Kusini, Gwede Mantash, kabla ya chakula cha jioni
alichowaandalia Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini
mwa Afrika, jana, Oktoba 9, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam, Makatibu
wakuu hao walikwenda Ikulu baada ya mkutano wao wa sita, uliofanyika
hapa nchini. Wapili kushoto ni Julio Paulo, Katibu Mkuu wa Chama cha
MPLA cha Angola na kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa wa Chama cha Kikomunisti cha China, Ai Ping na Katibu Mkuu
wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika,
kabla ya kula nao chakula cha jioni, Ikulu jijini Dar es Salaam, Oktoba
9, 2013. Kutoka kushoto na vyama vyao vikiwa kwenye mabano makatibu
wakuu hao ni, Nangolo Mbumba (SWAPO) cha Namibia, Gwede Mantash (ANC)
cha Afrika Kusini, Didy Mutasa (ZANU-PF) Zimbabwe, na kutoka kulia ni
Abdulrahman Kinana (CCM) Tanzania, Philipe Paunde (FRELIMO) Msumbiji na
Julio Paulo (MPLA) Angola.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akisisitizia jambo, Makatibu
Wakuu wa vyama vilivyokuwa vya Ukombozi Kusini Mwa Afrika, alipokutaja
nao kwa ajili ya chakula cha jioni, alichowaandalia, jana, Oktoba 9,
2013, Ikulu jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto na vyama vyao vikiwa
kwenye mabano makatibu wakuu hao ni Gwede Mantash (ANC) cha Afrika
Kusini, Didy Mutasa (ZANU-PF) Zimbabwe, na kutoka kulia ni Abdulrahman
Kinana (CCM) Tanzania, Philipe Paunde (FRELIMO) Msumbiji na Julio Paulo
(MPLA) Angola.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na ujumbe wa
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika,
wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam,
jana, Oktoba 9, 2013.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akizungumza na ujumbe wa
Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika,
wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia Ikulu jijini Dar es Salaam,
jana, Oktoba 9, 2013.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na Katibu wa NEC, Uchumi na
Fedha, CCM, Zakiah Meghji, wakati wa chakula cha jioni alichowaandalia
makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika,
jana, Oktoba 9, 2013, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimtambulisha Katibu
Mkuu wa Chama Cha MPLA cha Angola, Julio Paulo, kwa Makamu Mwenyekiti
wa CCM (Bara), Philip Mangula, wakati wa chakula cha jioni
kilichoandaliwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini
Dar es Salaam, jana, Oktoba 9, 2013.
Katibu Mkuu wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC, Gwede Mantash
(kushoto) akimpa zawadi, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana,
mwishoni mwa mkutano wa sita wa Makatibu wakuu wa vyama vilivyokuwa vya
ukombozi kusini mwa Afrika, jana, Oktoba 9, 2013, jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipewa zawadi Katibu Mkuu wa
chama cha SWAPO cha Naimibia Nangolo Mbumba, mwishoni mwa mkutano wa
sita wa vyama vilivyokuwa vya ukombozi kusini mwa Afrika, jana, Oktoba
9, 2013, jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni