KAMANDA
wa Polisi wa Kanda Maalum jijini Dar es Salaam, Suleiman
Kovaakizungumza na waandishi wa habari leo kwenye hospitali ya
Muhimbili.
…………………………………………………………………………………….
KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalum
jijini Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema hali ya mwandishi wa habari
wa ITV Ufoo Salo aliyepigwa risasi na mchumba wake Ancel Mush,
inaendelea vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini leo, Kova alisema tukio
hilo linahusishwa na ugonmvi wa kifamilia ambao hadi sasa haujafahamika
chanzo chake. Kwa mujibu wa madaktari, hali ya mgonjwa ilikuwa inaendelea
vizuri na alikuwa akitarajiwa kuingizwa chumba cha upasuaji nyakati za
mchana jana
Akizungumzia
mauaji hayo, Kova alisema japo mhusika alijiua
baada ya kumuua Anastazia Salo (58), bado kitendo hicho hakiliondolei
jeshi hilo haki kuchunguza kwa sababu inawezekana wapo waliyosbabisha
hadi mauaji kutokea. Kova alisema wanatarajia Ufoo atakuwa miongini mwa
watu watakaolisaidia jeshi hilo kupata taari zaidi za tukio la mauaji
hayo.
Ofisa
Mpelelezi wa Makosa ya Jinai, Ahmed Msangi alisema hasi
sasa hakuna taarifa kamili bali alichoweza kusema ni kwamba jeshi
limejigawa sehemu tatu ambpo kila kundi lilikuwa likikusanya taarifa.
Alisema alisema baada ya makundi hayo ambayo yalikuwa katika
maeneo ya nyumbani lilikotokea tukio, Tumbi hospitali na Muhimbili,
yatakusanya taarifa na kuzitoa kwa waandishi wa habari.
Reginald Mengi, alisema kipindi hicho Madaktari walikuwa
wakiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kukamilisha upasuaji “Hali yake
sio
mbaya inaendelea vizuri akiwa chini ya madaktari”alisema Mengi. Alisema
wanatarajia taarifa zaidi zitatolewa na msemaji wa hospitali hiyo ya
Taifa Muhimbili.
0 comments:
Chapisha Maoni