Searching...
Jumatano, 30 Oktoba 2013

BAJAJI YA MIZIGO YAPATA AJALI YA KUTISHA MWANZA

Ni bajaji ya mizigo ambayo ilikuwa na mizigo ya mafuta ya kula, chumvi, sabuni pamoja na unga imekula mzinga ikiovateki roli na kukuta roli upande wa pili limepaki na dreva wa bajaji alipojaribu kurejea kwenye upande wake wa kushoto ndipo breki zikamzidia akajibamiza nyuma ya roli alilokuwa akiliovateki...!!!
Wananchi waliofurika baada ya ajali hiyo kama sehemu ya mashuhuda.
Dereva wa bajaji hilo la mizigo aligonga nyuma ya roli hili la vyuma kama linavyoonekana upande wa kushoto.
Bahari ya mafuta ya kula....
Dereva wa bajaji hii alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando kupatiwa matibabu mara baaada ya kupata majeraha makubwa ya kutisha huku akimuacha mwenye mali ambaye alikuwa amepakizwa nyuma na mizigo akiwa amelowa mafuta na akiwa hana hata jeraha moja.
Taswira kamili na wananchi mashuhuda.
Hii ndiyo mizigo iliyosalimika wakati ile ya mafuta yooooote yakimwagika kupitia ajali hiyo.
Mizigo ikiwa imemwagika chini baada ya bajaji hiyo kupata ajali.
Askari wa jeshi la polisi Mwanza wakipima ajali hiyo. 

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!