TAHADHARI KWA PICHA ZIFUATAZO KWANI ZINATISHA
![]() |
Kiganja cha binadamu |
WAGANGA
wawili wa jadi akiwemo mfanyabiashara mmoja, wamenaswa jijini Mwanza,
wakiwa na kiungo cha mkono wa kulia unaoamainika kuwa wa binaadamu.
Watuhumiwa
hao waalikamatwa jumatatu mchana majira ya saa 9 katika eneo la Ziwani na
Uwanja wa Ndege wa Mwanza, kufatia taarifa za raia wema na kisha jeshi
la polisi kuweka mtego kwa muda wa wiki nzima na hatimaye kufanikiwa.
![]() |
Kiganja hicho kilihifadhiwa ndani ya chungu. |
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo, akitihibitisha tukio
hilo, alisema kwamba mkono huo uliokuwa umewekwaa kwenye begi na ambamo
ulikuwa umefungwa kwenye kwenye mfuko mweusi wa plasitiki na
kuviringishwa kwenye kalatasi nyeupe ya nailoni, umekutwa ukiwa mbichi.
Konyo
ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Mwanza (RCO),
alieleza kuwa watuhumiwa hao (majina yanahifadhiwa) wenye umri wa miaka
36 na 43 (ni waganga wa jadi wawili) na mfanyabiashara ana miaka 48.
Alisema
kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa katika jeshi hilo na kuweka
mtego huo kisha makubaliano ya kununua viungo hivyo kutoka kwa
watuhumiwa hao (wauzaji), walimhakikishia wanunuzi (polisi) kuwa
wanaweza kupata kichwa, mikono, miguu na sehemu za siri za binaadamu
endapo wangezihitaji.
“Taarifa
hizi ni za awali maana tukio lenyewe bado ni bichi kabisa na limetokea
muda mfupi uliopita hivyo taarifa zaidi tutazitoa baada ya kukukamilisha
upelelezi wetu ikiwa pamoja na kuwakamata watuhumiwa na kubaini
binaadamu aliyeuawa na kukatwa baadhi ya viungo ambavyo waganga hao
walidai wanaweza kuvipata.” Alieleza.
Alieleza
akwamba, kwa mujibu wa makubaliano hayo, wauzaji hao walkitaka kupewa
sh milioni 100 kwa mkono huo mmoja lakini baada ya kufanya mazungumzo ya
kibiashara na wao kuona kitita cha fedha, walilegeza bei na kujikuta
wakitiwa mbaroni baada ya kuonyesha kiungo hicho.
![]() |
Ulinzi uliimarishwa katika eneo hili kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa. |
Kamanda
Konyo pamoja na kuwapongeza wananchi waliotoa taarifa zilizofanikisha
mtego huo, alisema jeshi lake liko katika harakati za kupambana na
mauaji na uhalifu wa kila aambapo tayari kikosi kazi kiko katika wilaya
ya Magu kikishirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kinawatia
mbaroni watu wanaojihusisha na uhalifu na mauaji.
![]() |
Wananchi wakiwa katika hali ya kutafakari juu ya tukio hilo la kusisimua. |
![]() |
Bado ni mshangao kwa kila aliyefika eneo hili la kituo cha polisi Air Port Mwanza. |
![]() |
Watuhumiwa wakiwa na kiganja hicho cha binadamu. |
![]() |
Maafisa wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza wakiwaongoza watuhumiwa kuelekea eneo la usalama kwaajili ya mahojiano zaidi. |
![]() |
Wananchi na wafanyakazi wa Airport Mwanza wakiwa ma maswali juu ya sakata hilo. |
![]() |
Mara baada ya watuhumiwa hao kuondoshwa toka katika kituo cha polisi Airport Mwanza walifikishwa kituo cha polisi Kirumba kwaajili ya hatua nyingine za kisheria. |
![]() |
Kitupo cha polisi Kirumba jijini Mwanza. KWA HISANI YA G SENGO BLOG. |
0 comments:
Chapisha Maoni