Searching...
Jumapili, 22 Septemba 2013

WALIOFARIKI KATIKA SHAMBULIO LA KENYA WAFIKIA 59,MSAKO MKALI UNAENDELEA NDANI YA DUKA HILO KUWASAKA MAGAIDI WALIOSHAMBULIA.

 Askari wa kenya akiwa katika msako mkali wa kuwatafuta magaidi waliolipua kwa kushambulia watu jana katika duka moja la kifahari la westgate jijini Nairobi ambapo hadi sahivi imeripotiwa kwamba watu 59 wamekufa kama mmoja wa mwili wa marehemu unavyoonekana hapo pembeni aliyeuwawa katika shambulio hilo huku wengine 162 wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
 msako mkali ukiendelea leo asubuhi kuwasaka magaidi ambapo serikali ya kenya wanaamini kwamba watu hao walioshambulia bado wapo ndani ya duka hilo.
 makamanda wapo kazini mpaka magaidi wapatikane.
 mwendo wa ku-crow!! waliopitia vyombo vya ukakamavu huu mwendo wanaujua.
unaweza ukafikiri ni sinema ya Van Dame au Jack Chein lakini ni makamanda wa vita wa Kenya wakiwa kazini kuwasaka magaidi kila kona ndani ya duka hilo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!