GARETH BALE-REAL MADRID.
Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Brazil na timu ya Real Madrid Ronaldo De Lima amempa onyo kali mchezaji ghali duniani kwa sasa aliyejiunga na miamba ya soka ya Hispania Gareth Bale kwamba kitendo cha yeye kuwa mchezaji ghali duniani kisije kikamvimbisha kichwa.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Real Madrid,ambaye alisajiliwa kwa kitita cha paundi milioni 22 mwaka 2002, amemtaka Bale kujiona kama hajui kitu na aendelee kujifunza,vinginevyo hatadumu Madrid.
‘Ni lazima ajue kwamba pale atakapocheza chini ya kiwango,ni lazima mashabiki watajiuliza kama huyu kweli ndiye mchezaji aliyenunuliwa kwa paundi milioni 86 na kuvunja rekodi ya dunia?,’ Alisema Ronaldo.
‘ninachoweza kumuasa Bale ni kwamba lazima ajitahidi kucheza vizuri ili asiipoteze thamani yake.’RONALDO DE LIMA.CHRISTIAN RONALDO
Wachambuzi wa masuala ya soka wanasema itamlazimu Bale kushindana na Cristiano
Ronaldo kama atataka kuonyesha thamani yake halisi,japokuwa amesema daima anamuheshimu Ronaldo na anatarajia kujifunza mengi kutoka kwake.
0 comments:
Chapisha Maoni