Hivi vilikua ni vita kati ya Upinzani na Askari polisi wa Bunge ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
|
Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai
akimwamuru Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe kukaa chini, Bungeni
Mjini Dodoma Septemba 5, 2013.
|
|
Wabunge wa Chadema wakiwa wamesimama
kukaidi amri ya Naibu spika, Job Ndugai ya kuwataka wakae chini , Bungeni
Septemba 5, 2013. |
Wabunge wa CUF na Chadema wakiwa wamemzunguka mheshimiwa Mbowe ili asitolewe nje na polisi
|
Wabunge wa CUF na CHADEMA wakipambana na
Polisi, Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5,2013. |
|
Mbunge wa Kuteuliwa na
Mwenyekiti wa NCCR_MAGEUZI, James Mbatia akishangaa kuona mapambano kati ya
wabunge wa CHADEMA na Polisi Bungeni Septemba 5, 2013. |
Nguvu ya polisi ikaanza kutumika
|
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa
ameng'ang'ania Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni
wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma Septemba 5, 2013.
Hata hivyo Microphone hiyo iling'oka na polisi wakafanikiwa kumtoa nje ya ukumbi wa bunge. |
|
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akitolewa na Askari Polisi nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Septemba 5, 2013. |
Askari 7 wakijiandaa kumbeba juu juu mheshimiwa Mbilinyi
Hatimaye kwa busara mheshimiwa Mbowe akaamua kutoka nje bila polisi kumgusa
Mbowe anachekaaaa
|
Kiongozi wa Upinzani
Bungeni, Freeman Mbowe akiongoza wabunge wa CHADEMA kutoka Bungeni mjini Dodoma baada ya kuamriwa
kufanya hivyo na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai Septemba 5, 2013. |
|
Mbunge wa Mbeya Mjini
akizuiwa na wabunge wa CHADEMA ili asipambane na polisi, Bungeni
Mjini Dodoma Septemba 5, 2013. |
0 comments:
Chapisha Maoni