Aliyejidai kuwa ni Daktari katika hosptali ya KCMC(Daktari Feki) aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe akiwa amefungwa pingu mikononi mwake katika eneo la hosptali hiyo.
Afisa uhusiano wa hosptali ya Rufaa ya KCMC,Gabriel Chisseo akimwonesha anayedaiwa kujifanya daktari katika hosptali hiyo (Daktari Feki) aliyetambulika kwa jina la Alex Massawe.
Daktari Feki Masawe akisindikizwa na baadhi ya wafanyakazi wa hosptali ya KCMC kutoka katika moja ya wodi ambayo alikuwa ‘akihudumia’.
Daktari feki akiwa katika gari la polisi tayari kupelekwa kituo cha polisi ili hatua za kisheria zichukuliwe
Na Dixon Busagaga, Moshi.
HALI
ya wasiwasi imetanda kwa baadhi ya wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika
Hospitali ya Rufaa ya KCMC ya mjini Moshi baada ya uongozi wa hospitali
hiyo kumkamata mtu mmoja anayedaiwa kujifanya ni daktari wa watoto
akiwa kwenye wodi ya upasuaji.
Daktari
huyo feki aliyefahamika kwa jina la , Alex Sumni Massawe alikamatwa
jana majira ya saa 5 asubuhi na kuwekwa chini ya ulinzi mkali wa
makachero wa Jeshi la Polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia baada ya
kukutana na mmoja wa wagonjwa ambaye alimuahidi kumfanyia mwanae wa
kiume upasuaji wa ngozi.
Kabla
ya kukamatwa kwa Alex, mama mzazi wa kijana aliyekuwa akitakiwa
kufanyiwa upasuaji, Pamvelina Shirima alikutana na daktari huyo katika
baa moja maarufu mjini hapa iliyopo eneo la Dar Street (jina
limehifadhiwa) na kumtoza sh.200,000 akidai zitatumika kuharakisha
mwanae afanyiwe vipimo vya upasuaji.
Alex
anadaiwa alitaka kumfanyia upasuaji kijana, Makasi Tipesa, mkazi wa
Manispaa ya Moshi ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi kwa
muda mrefu sasa.
Ofisa
Uhusiano wa Hospitali ya KCMC, Bw. Gabriel Chisseo alisema daktari huyo
aliwekewa mtego na uongozi wa hospitali ya KCMC kutokana na baadhi ya
wagonjwa kuripoti kutapeliwa na mmoja wa madaktari ambaye amekuwa
akijinasibu kwamba anafanya huduma hiyo kutokana na wito alionao katika
fani hiyo.
“Leo
asubuhi(jana) mteja wetu ambaye amekuwa akitibiwa hapa alitapeliwa na
huyu Alex , tulimkamata akiwa wodi ya upasuaji baada ya kupokea kiasi
cha sh.200,000 kutoka kwa Pamvelina Shirima ambaye alimleta mwanae
afanyiwe upasuaji wa ngozi”, alisema Chisseo.
Uongozi
wa Hospitali ya KCMC umethibitisha kwamba mtu huyo aliyekamatwa ndani
ya Hospitali hiyo, si mwajiriwa wao na wala hakukutwa na sare wala
kitambulisho kinachomtambulisha kitengo chake cha kazi.
Hivi
karibu kumeibuka matukio ya watu kadhaa kujivika kuwa na taaluma
mbalimbali ambazo si za kweli huku jeshi la polisi likifanikiwa
kuwakamata wengine wakijifanya kuwa ni maofisa wa jeshi hilo ,wengine
usalama wa taifa huku wengine wakijifanya asakri wa kikosi cha usalama
barabarani
0 comments:
Chapisha Maoni