Raia mmoja wa Canada amekamatwa nchini Colombia baada ya kujaribu kupanda ndege kurejea Canada akiwa na tumbo la ujauzito bandia ambapo ndani yake alikua ameficha dawa za kulevya aina ya Cocaine.
Mwanamke
huyo aliyekuwa anajifanya kuwa mtalii akirejea Toronto, alihojiwa na
polisi katika uwanjwa wa ndege wa Bogota aliyemshuku na kumuuliza
alikuwa amesalia na miezi mingapi kujifungua.
Alijibu kwa ukali mno , hali iliyomfanya afisaa huyo kumshuku sana na hivyo kumfanyia ukaguzi zaidi.
Afisaa huyo aligusa tumbo lake na kuhisi lilikuwa baridi mno na gumu sana ndipo wakaamua kumkagua zaidi.
walimpata
na dawa za kulevya zilizokuwa zimefungwa ndani ya tumbo bandia ya mimba
ambayo mwanamke huyo alikuwa ameivaa kwa kufunga tumboni.
Inasemekana
kuwa alisema ana miezi saba ya ujauzito lakini baada ya polisi kumkagua
walimpata na Cocaine kilo mbili iliyokuwa ndani ya vipochi viwili
Mwanamke huyo atashtakiwa kwa kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya na huenda akafungwa jela kwa miaka mitano au nane.
Mwaka huu pekee karibu watu 150 wamekamatwa na dawa za kulevya katika uwanja wa ndege wa Bogota.
Karibu thuluthi moja kati ya waliokamatwa walikuwa raia wa kigeni, kwa mujibu wa maafisa wakuu nchini Colombia.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.