Gari aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa limewabeba maofisa wa wizara ya nishati na madini kitengo cha wakala wa umeme vijijini REA wakiwa katika msafara wa waziri wa wizara ya nishati na madini Mheshimiwa Profesa Sospeter Muhongo likiwa kichwa chini miguu juu.
Baadhi ya wafanyakazi wa wizara ya nishati na madini wakiwashuhudia maofisa hao wakitolewa ndani ya gari hili,ajali iliyotokea kijiji cha Butata Musoma vijijini ambapo chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa ni vumbi kubwa lililokuwa likitimka katika msafara huo.
Wasamaria wema wakiwa pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa wizara hiyo waliokuwepo katika ziara hiyo wakiwatoa majeruhi hao na kisha kuwakimbiza hosiptalini kwaajili ya matibabu.
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.