Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi
wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa
wa Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji
kazi wa idara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame
Silima. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak
Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester
Ambokile Mwakinyule. Dk Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa
uadilifu. Mkutano huo ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu,
jijini Dar es Salaam leo. (Picha na
Felix Mwagara, Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na watumishi
wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa idara hiyo Mkoa
wa Dar es Salaam. Dk Nchimbi alifanya ziara ya siku moja
katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam
leo kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao masuala mbalimbali ya
utendaji kazi.. (Picha na Felix
Mwagara, Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).
Kamishna wa Pasipoti na Uraia, wa Idara
ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto) akimuuliza swali Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (wa pili kutoka kulia) kuhusu
masuala mbalimbali ya maendeleo ya idara hiyo. Watumishi mbalimbali waliuliza
maswali pamoja na kutoa maoni yao katika mkutano huo uliofanyika katika
Ofisi za Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Kulia
ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto (Meza Kuu) ni
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja
na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile
Mwakinyule. (Picha na Felix Mwagara,
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).
0 comments:
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.