Searching...
Jumatatu, 2 Septemba 2013

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA 6 ABUNI NJIA YA KUPIGA KURA KWA NJIA YA MTANDAO


Mwanafunzi Wycklif Michael anayesoma kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Loyola, akimuonesha Naibu Waziri Mulugo programu ya mfumo wa kupiga kura aliyoibuni.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo akimuangalia mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Premier Rehema Ng’anzi,  anayeonesha kwa vitendo mambo ya kisayansi wanayosoma shuleni kwao, wakati alipotembelea banda la shule hiyo kwenye maonesho ya Vodacom Elimu Expro.
Naibu Waziri Mulugo akimsikiliza Mkurugenzi wa JUE INTER SCHOOLS Ester Alexander kutoka Arusha wakati  akimueleza juu mambo yanayofanywa na shule yake.
Elizabeth Thomas (aliyeshika kipaza sauti) kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala akimueleza Naibu  Waziri Mulugo kuhusu Tamasha la Mnazi Mkinda  linaloandaliwa na halmashauri hiyo kuboresha sekta ya elimu katika eneo hilo.
Naibu Waziri Mulugo akipiga kinanda kwenye banda la Shule ya Sekondari ya Green Acres wakati alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Vodacom Elimu Expro.
Na Hussein Makame

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!