Meli
iitwayo Gold Star imekamatwa karibu na pwani ya Italia ikiwa na zaidi ya
tani 30 za dawa za kulevya ambapo Polisi wa Italia wamesema documents
zinaonesha ilisajiliwa Tanzania.
Taarifa nyingine ya polisi imesema mzigo huo una thamani ya poundi
millioni 50 ambayo kwa pesa za kitanzania ni kama 126,582,278,481 na
meli yenyewe ilikua na timu ya watu tisa ambao wanatoka Misri na Syria
na mzigo wote wameupakia kutoka Uturuki.
Unaambiwa baada ya kuona mchezo wao umefahamika, watu waliokuwemo kwenye meli waliamua kuanza kuichoma moto meli hiyo na wote tisa walijirusha baharini kwa nia ya kutaka kukimbia lakini wakakamatwa mapema tu na kukutwa na hizo dawa za kulevya aina ya hashish ambazo thamani yake inagonga kwenye £Paundi milioni 50.
Bandari husika ya Italia walipewa taarifa kwa siri mapema siku kadhaa
kwamba meli hii ilikua imebeba tani nyingi za dawa za kulevya hivyo
wakawa wanaifuatilia kwa siku kadhaa kabla ya kuikamata.
Msemaji wa bandari amesema hawakutegemea kama meli hiyo ingekua
imebeba kiasi hicho cha dawa za kulevya na pia hawakutegemea kama watu
waliokuwemo ndani yake wangeichoma moto ili kupoteza ushahidi japo zoezi
hilo halikufanikiwa na dawa zikaonekana.
Meli hiyo imesogezwa kabisa mpaka kwenye bandari na moto umezimwa
huku msako zaidi ukiendelea kwenye sehemu nyingine za meli hiyo ili
kuona kama kuna dawa nyingine za kulevya huku watu wote tisa wakiwa
wanaendelea kuhojiwa.
CHANZO: MILLARD AYO
0 comments:
Chapisha Maoni