Searching...
Jumatatu, 16 Septemba 2013

MBUNGE WA CHADEMA APAMBA MKUTANO WA CCM MEATU,AWAMWAGIA SIFA KINANA NA NAPE

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mbunge wa CHADEMA jimbo la Maswa Magharibi Mh. John Shibuda wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu, ambapo ameelezea kuwa Siasa siyo ugonvi na alikuja Meatu kwa sababu mbili tu Moja ilikuwa ni kukutana na Ndugu Kinana kwa ajili ya kujadiliana mambo mbalimbali juu ya tatizo la zao la Pamba kuhusu bei ya zao hilo na matatizo ya pembejeo kwa wakulima wa Wilaya hiyo, Akaaongeza kwamba jambo la pili ni kwamna Ndugu Abdulrahman Kinana ni rafiki yake wa muda mrefu kwa hata wakati wakisoma shule wote walisoma moshi Abdulrahman Kinana akisoma Old Moshi Sekondari na John Shibuda Mwenyewe akisoma Moshi Technical lakini pia akasema wakati alipokuwa akigombea ubunge wa Maswa Magharibi Kinana alimchangia shilingi Milioni moja "Siasa nia Siyo Matusi ni Ushirikiano na kukosoana kwa hoja" amemaliza Shibuda. 3Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo katika mkutano huo huku Mbunge wa jimbo la Maswa Magharibi John Shibuda akimsiliza, kushoto anayetabasam ni Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye. 4 Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano huo kushoto ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA. 5 Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi Nape Nnauye akikumbatiana kwa furaha na John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA mara baada ya kupanda jukwaani katika viwanja vya Meatu mjini, kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuhudia. 6Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi CHADEMA Mh John Shibuda akiwasili katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika kwenye viwanja vya Meatu mjini Meatu leo huku vijana wa Chama chaCHADEMA wakimsindikiza.. 

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!