Mjapani huyo alifunguka muda mfupi baada ya kuifungia timu yake goli zuri timu yake ya taifa katika ushindi wa magoli 3-1 dhidi timu ya taifa ya Ghana ambapo waandishi wa habari walimuuliza kwanini tangu msimu huu uanze amecheza dakika tisa tu?
Mashabiki wa Manchester United wamekua wakimshangaa kocha wao kwa kumuacha nje ya kikosi chake mchezaji mdogo wa miaka 24 ambaye anaonekana kuwa na uwezo mkubwa na kipaji cha ajabu ambapo pia ashawahi kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Ujerumani mara mbili wakati akiichezea klabu ya Borussia Dortmund.
‘Tafadhalini sana swali hilo muulizeni David Moyes kwamba kwanini sipo kwenye mipango yake,
‘Inanichanganya sana kwanini sichezi Manchester United,lakini kufunga goli zuri kama hili kwangu ni faraja na pia inanipa hali ya kujiamini zaidi.
Kufuatia Mchezo mzuri aliouonyesha katika timu yake ya taifa Kagawa atakua amemshawishi kocha wake kumpa nafasi katika kikosi chake Old Trafford.
‘Inauma sana kwa mchezaji mzuri kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara,lakini imekua vizuri kwangu kurejea timu ya taifa na kupata nafasi ya kucheza na kisha kufunga goli na kuipa timu yangu ushindi....nilikosa goli moja katika kipindi cha kwanza na ndio maana nilipopata nafasi ya kufunga kwa mara ya pili sikutaka kuipoteza,’alifunguka Shinji Kagawa
Katika hali ya kuonekana kutokukubaliana na jinsi David Moyes alivyoianza ligi kuu ya England kwa mara ya kwanza akiwa na miamba ya soka Manchester United kocha wa zamani wa klabu hiyo ambaye bado ni sehemu ya klabu hiyo licha ya kuachia ngazi Sir Alex Ferguson amesema siri kubwa ya yeye kuwa kocha bora katika ligi kuu ya England ni kutokana na ujasri wake wa kuwa tayari kwa lolote "risk taker" akizungumza na waandishi wa habari Ferguson amesema yeye alikua pale anapokuwa nyuma dakika 15 za mwisho alikua yupo tayari kutoa mabeki na kuingiza washambuliaji zaidiili kubadilisha matokeo.
‘mimi nilikua tayari kwa lolote "a risk taker" pale timu ilipokuwa imefungwa na mara nyingi nilikua nikipata matokeo mazuri na watu kushangaa,nilikua naamini ni bora tufungwe magoli 3-2 kuliko kufungwa magoli 3-1"alimalizia Babu Fergie.
0 comments:
Chapisha Maoni