Rais
Jakaya Kikwete akisisitiza jambo wakati akisomewa taarifa ya Wilaya ya
Kwimba na Mkuu wa Wilaya hiyo Ndugu Seleman Mzee huko Ngudu makao makuu
ya wilaya tarehe 9.9.2013.
Rais
Jakaya Kikwete akipokewa kwa shangwe na hoihoi wakati alipowasili
kwenye Chuo cha Michezo Malya kilichoko wilayani Kwimba tarehe 9.9.2013.
Rais
Jakaya Kikwete akipokea taarifa ya ujenzi wa uwanja wa ndani wa michezo
wa chuo cha michezo cha Malya kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Ndugu Allen
Allex. Rais Kikwete baadaye aliufungua rami uwanja huo.
Rais
Jakaya Kikwete akizindua rasmi uwanja wa ndani wa michezo kwa kukata
utepe. Walioshika utepe huo kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Malya
Ndugu Allen Alex, Dkt. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana,
Utamadunu na Michezo, Ndugu Richard Ndassa, Mbunge wa Sumve na wa mwisho
ni Mbunge wa Kwimba.
Mkuu
wa Chuo cha Michezo cha Malya Ndugu Allen Alex akimwelezea rais Jakaya
Kikwete ramani ya eneo lote la chuo mara tu baada ya uzinduzi wa uwanja
wa ndani wa michezo.
Rais
Jakaya Kikwete akipokewa kwa shangwe na hoihoi wakati alipowasili
kwenye Chuo cha Michezo Malya kilichoko wilayani Kwimba tarehe 9.9.2013.
Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kituo cha polisi cha wilaya ya Kwimba mjini Ngudu tarehe 9.9.2013.
Mheshimiwa
Rais Jakaya Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni wa Kisukuma
zilizokuwa zikicheza wakati Rais Jakaya Kikwete alipofika tu uwanjani
hapo kwa ajili ya mkutano wa hadhara huko Ngudu tarehe 9.9.2013.
Rais Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi wa Ngudu muda bmfupi kabla ya kuwahutubia.
Rais
Jakaya Kikwete akiangalia na kupata maelezo ya mchoro wa mtandao wa
maji katika mkoa wa Mwanza yaliyokuwa yakitolewa na Waziri wa Maji
Profesa Jumanne Maghembe wakati wa mkutano wa hadhara mjini Ngudu.
Rais
Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti na fedha taslim shilingi laki tano
Muuguzi wa hospitali ya wilaya ya Kwimba ndugu Rhoda Joseph Michael
kutoka kwa mkuu wa wilaya baada ya muuguzi huyo pamoja na daktari Makori
Josephat Maro kuamua kutoa damu yao kwa ajili ya mama aliyekuwa
mjamzito na kuwa na upungufu wa damu wakati wa kujifungua baada ya ndugu
wa mama huyo kushindwa kupata damu inayofanana naye. Rais Kikwete
aliwazawadia sh milioni moja na nusu kila moja kwa kitendo hicho. Picha
ya pili Rais Kikwete akimpongeza daktari huyo.
Rais
Jakaya Kikwete akiwahutubia mamia ya wananchi wa Kwimba huko mjini
Ngudu ili kuhitimisha ziara ya ya siku moja wilayani humo tarehe
9.9.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI
0 comments:
Chapisha Maoni