Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akila pamoja na wananchi wa tawi la Isenge kata ya Dutwa baada ya kushiriki nao ubebaji wa matofali na uchimbaji wa msingi wa nyumba ya Balozi.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus
Kamani,Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Pascal Mabiti na Mbunge wa Bariadi Andrew
Chenge wakila chakula cha Asili aina ya Michembe pamoja na Balozi Joyce
Safari wa Shina namba 12 kata ya Dutwa.Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimimina maharage kwenye wali uliokuwa kwenye tayari kula na wananchi pamoja na viongozi wengine.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kubeba matofali kwa ajili ya
ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari wa shina namba 12 tawi la
Isenge kata ya Dutwa.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
Nape Nnauye wakichimba msingi wa ujenzi wa nyumba ya balozi Joyce Safari
wa shina namba 12 Tawi la Isenge kata ya Dutwa.




0 comments:
Chapisha Maoni