MIILI YA ASKARI HAO IKIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KAHAMA
Askari
Polisi watatu wa operesheni Kimbunga ya kusafisha wahamiaji haramu nchini,
wamefariki dunia jioni hii mjini Kahama kufutia ajali ya gari walilokuwa
wakisafiria kutoka Muleba mkoani Kagera kuelekea makambako mkoani Njombe.
Marehemu
hao waliotambulika kwa majina ya Kopolo Fred,PC Subian na PC Michael wote ni
askari wa kituo cha Polisi Makambako, na mauti yamewafika baada ya gari nambari
PT 0776 Land Rover Diffender kuacha njia na kupinduka.
Ajali
hiyo imetokea katika eneo la Sungamile Kata ya Kagongwa wilayani Kahama wakati
dereva wa gari hilo PF3270 PC Yusuph, akijaribu kumkwepa Bibi Kizee mmoja huku
gari likiwa kwenye mwendo kasi hali iliyosababisha kumshinda na kupinduka.
Kijukuu Blog imeshuhudia Majeruhi wanane wakilazwa katika Hospitali ya wilaya ya
Kahama wakiwemo askari polisi sita na Afisa uhamiaji wawili, huku magari
yanayosafirisha askari kurudi vituoni kwao yakizuiliwa kuendelea na safari na
kulala Kahama.
Kumbukumbu
za kipolisi pia zimeonesha kuwa hapo jana jioni askari wengine walipata ajali
katika kijiji cha Igusule wilayani nzega ambapo askari 4 wamelazwa katika hospitali
ya wilaya Kahama huku mmoja akiwa na hali mbaya.
Oparesheni
Kimbuga ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete, la kuwaondoa wahamiaji
haramu nchini, ambapo vikosi vya ulinzi kwa pamoja viliunda kikosi kimoja na
kufanya kazi nchini kote.
0 comments:
Chapisha Maoni