Searching...
Alhamisi, 5 Septemba 2013

.................BREAKING NEWSSSSS.......

Taarifa ambazo tumezipata hivi punde zinasema mamia ya wasafiri waliokua wanasafiri kutoka jijini Dar es salaam kwenda mikoani na nchi za jirani kupitia barabara ya Morogoro wamekwama barabarani kwa takribani saa mbili kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha malori mawili alfajiri  ya leo na kisha kulalia barabarani na kufunga njia.
akizungumza na MCHOME BLOG mmoja wa askari wa barabarani ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa kuwa yeye sio msemaji wa jeshi hilo amesema ajali hiyo imetokea maeneo ya kati kati ya vijiji vya Pingo na Chamakweza kati ya Mlandizi na Chalinze na chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa lori hilo ambapo pia lilikua lina taa hafifu na kushindwa kuliona lori lingine lililokuwa limepaki barabarani baada ya kuharibika.
Hata hivyo hakuna mtu aliyejeruhiwa wala kupoteza maisha katika ajali hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni

 
Back to top!