Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akiwa na
Balozi wa China nchini, Lu Youqing walipokuwa wakikagua mitambo ya
kisasa ya kuunganisha mabomba ya kusafirishia gesi, katika karakana
namba tano ya Kampuni ya kichina ya CPTDC ya Ikwiriri, wilayani Rufiji,
Mkoa wa Pwani .Profesa Muhongo alifanya ziara ya siku moja ya kukagua
utekelezaji wa maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia)
akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya kichina ya CPTDC
iliyopewa tenda ya kutandaza mabomba ya gesi kutoka Mtwara hadi Dar es
Salaam, alipokuwa katika ziara ya siku moja ya kukagua utekelezaji wa
maandalizi ya utandazaji wa mabomba hayo ya gesi, juzi eneo la Somanga
Fungu, wilayani Kilwa, Mkoa wa Lindi.
Sehemu ya mabomba ya gesi yakiwa eneo la kuhifadhia la Nyamwage, Rufiji
Profesa Muhongo akiangalia kipenyo cha bomba ambacho ni mita moja
Profesa Muhongo akioneshwa sehemu ya bomba itakayounganishwa na bomba lingine
Watalaamu wa ubora wa ufungaji mabomba ya gesi kutoka Afrika Kusini
wakimueleza Waziri Muhongo kuhusu umakini wakati wa kuunganisha mabomba
hayo
Profesa Muhongo akiwa eneo la kuhifadhia mabaomba, Nyamwage, wilayani Rufiji. Mabomba hayo yalianza kuunganishwa jana.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia),
akizungumza na baadhi ya vibarua wa kitanzania wanaofanya kazi katika
kampuni hiyo ya kichina katika kambi ya kuhifadhia mabomba ya Nyamwage,
wilayani Rufiji, Pwani.
Waziri Muhongo akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kamapuni hiyo ya kichina.
Kambi ya wafanyakazi wa kampuni ya kichina eneo la Mkuranga, Dar es Salaam
Waandishi wa habari walioambatana na Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo (amezibwa), wakiangalia nyaya za mkongo
zitakazotandazwa sambamba na mabomba ya gesi kwa ajili ya usalama,
zilizokuwa kwenye lori katika ghala la kampuni hiyo ya kichina wilayani
Mkuranga, Pwani
Baadhi ya mitambo ikiwa imefungwa wilayani Mkuranga, Pwani, kwa ajili ya
kuongezea unene wa mabomba maalumu ya gesi yatakayotandazwa
baharini.
PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO
BLOG.
0 comments:
Chapisha Maoni